RAIS AJAE ATAKIWA KUWA KIONGOZI MWENYE KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU

RAIS AJAE ATAKIWA KUWA KIONGOZI MWENYE KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU

Like
301
0
Thursday, 04 June 2015
Local News

UMOJA wa mabadiliko ya walimu Tanzania –VUMAWATA umemwomba rais ajae awe kiongozi ambae ataweza kutatua  changamoto mbalimbali zinazo wakabili walimu hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti Taifa wa Umoja huo ALLY MAKWIRO amesema kuwa changamoto za walimu zimekuwa ni kitu cha kawaida na hazijapata suluhisho la kudumu mpaka sasa kitu ambacho kinasababisha walimu kuwa masikini na kutokuwa na hadhi katika nchi na jamii kwa ujumla.

MAKWIRO amesema kuwa walimu wana changamoto nyingi katika maisha yao ikiwemo kufanyakazi katika mazingira magumu hasa walimu wa vijijini, uhaba wa vifaa vya kufundishia, ofisi zisizo kidhi vigezo kwaajili ya kazi yao.

Comments are closed.