RAIS AMTEUA DK. MATARAGIO KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TPDC

RAIS AMTEUA DK. MATARAGIO KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TPDC

Like
311
0
Thursday, 18 December 2014
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dokta James Mataragio kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania -TPDC.

 

Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.

 

Dokta Mataragio ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani.

 

Aidha, Dokta Mataragio pia ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.

 

Comments are closed.