Rais Donald Trump aonyesha nia ya kutoa ushahidi mbele ya mwendesha mashitaka maalum

Rais Donald Trump aonyesha nia ya kutoa ushahidi mbele ya mwendesha mashitaka maalum

Like
368
0
Friday, 23 March 2018
Global News

Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameonyesha nia ya kutoa ushahidi mbele ya mwendesha mashitaka maalum anayechunguza uingiliaji kati wa Russia katika uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016 na mambo mengine.

Ningependa Trump alijibu alipohojuiwa na waandishi wa habari kutaka kujua kama ana nia ya kuhojiwa na wachunguzi.

Rais alitoa jibu hilo wakati akiondoka katika chumba cha kidiplomasia cha White house mara tu baada ya kusaini nyaraka ya kuelekeza utawala wake kuchukua hatua za kibiashara dhidi ya China.

Majibu ya Trump yalikuja baada ya taarifa kwamba mmoja wa mawakili wake John Dowd kuthibitisha kwamba anajitoa.

Comments are closed.