RAIS FILIPE NYUSSI AKUTANA NA RAIA WA MSUMBIJI WAISHIO TANZANIA

RAIS FILIPE NYUSSI AKUTANA NA RAIA WA MSUMBIJI WAISHIO TANZANIA

Like
248
0
Monday, 18 May 2015
Local News

RAIS wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe  Nyussi ameendelea na ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania ambapo leo amekutana na Raia wa Msumbiji waishio nchini nakufanya nao mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa, uchumi na kijamii.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Mheshimiwa Filipe  Nyussi amesema Msumbiji na Tanzania ni ndugu wa karibu wa muda mrefu tokea enzi za mapambano ya uhuru wa nchi hiyo ambapo Tanzania iliwasaidia kikamilifu katika harakati za kudai uhuru wao.

Mheshimiwa Nyussi pia amebainisha kuwa Msumbiji ikiwa kama Taifa lililopata Rais mpya na kuanza mwanzo mpya ni lazima kufikiria ni wapi limetoka na wapi linakwenda.

 

Comments are closed.