RAIS JAKAYA KIKWETE ATEUA WAKUU WA TAASISI TOFAUTI SERIKALI NA MAHAKAMA

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEUA WAKUU WA TAASISI TOFAUTI SERIKALI NA MAHAKAMA

Like
284
0
Friday, 12 December 2014
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Laurence Nyasebwa Mafuru kuwa Msajili wa Hazina kuanzia tarehe 5 Novemba, 2014.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa -PDB.

Aidha Bwana Mafuru pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya uangalizi wa muda wa Benki Kuu ya Tanzania -BoT.

Comments are closed.