RAIS KIIR AKIMBIZWA HOSPITALINI ETHIOPIA

RAIS KIIR AKIMBIZWA HOSPITALINI ETHIOPIA

Like
270
0
Thursday, 29 January 2015
Global News

MKUTANO wa viongozi wa kikanda ulioandaliwa kujadili mgogoro wa mwaka mmoja ulioko nchini Sudan Kusini, umecheleweshwa baada ya Rais Salva Kiir kuugua na kukimbizwa hospitalini mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Afisa mmoja wa shirika la IGAD, ambalo linafanya juhudi za kuwakutanisha viongozi wa Sudan Kusini kwa lengo la kumaliza vita, ameliambia shirika la Utangazaji la BBC, kwamba Rais Kiir, alianza kuvuja damu kutoka puani.

Kabla ya kuugua, hapo jana Rais Kiir alifanya mazungumzo na kiongozi wa waasi Riek Machar ambapo alimtaka kutupilia mbali maswala yanayochochea mgogoro huo ili kumaliza mgogoro ambao umedumu mwaka mmoja sasa.

 

Comments are closed.