RAIS KIKWETE AANZA ZIARA NCHINI KENYA

RAIS KIKWETE AANZA ZIARA NCHINI KENYA

Like
748
0
Monday, 05 October 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ameanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika Jamhuri ya Kenya kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta ambako miongoni mwa shughuli atakazozifanya ni pamoja na kulihutubia Bunge la Kenya.

 

Rais Kikwete ameanza ziara yake jana kwa kuungana na Rais Kenyatta kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Taveta-Mwatate ambayo ni sehemu ya barabara inayounganisha Tanzania na Kenya ikianzia Arusha-Holili-Taveta-Mwatate.

 

Barabara hii itaunganisha eneo la kaskazini mwa Tanzania na Bandari ya Mombasa, Kenya.

 

 

RAIS2

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete eneo la TAVETA nchini Kenya muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili na kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.

RAIS1

Rais Kikwete akilakiwa kwa furaha na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto

 

Comments are closed.