RAIS KIKWETE AKABIDHI MISAADA KAMA ZAWADI KUSHEREHEKEA IDD ALHAJI

RAIS KIKWETE AKABIDHI MISAADA KAMA ZAWADI KUSHEREHEKEA IDD ALHAJI

Like
376
0
Wednesday, 23 September 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amekabidhi misaada yenye thamani ya shilingi milioni 9 na laki 7 kwa vituo mbalimbali vya makundi maalum Tanzania bara na Visiwani ikiwa kama zawadi ya kusherekea sikukuu ya Idd Alhaji inayotarajiwa kuwa kesho Septemba 24 mwaka huu.

Misaada hiyo iliyojumuisha mchele , mafuta ya kupikia na mbuzi vimegaiwa kwa vituo hivyo ili na wao waweze kusherekea na kufanikisha sikukuu za Idd kama watu wengine kwa kuwa sikukuu hiyo husherekewa kila mwaka na Waislam wote duniani baada ya kumaliza safari ya kuhiji Mecca nchini Saudi Arabia.

Comments are closed.