RAIS KIKWETE AKUTANA NA MUSEVENI MAREKANI

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MUSEVENI MAREKANI

Like
321
0
Friday, 25 September 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni mjini New York, ambapo wamezungumzia masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Uganda, yanayohusu Jumuia ya Afrika Mashariki ambako Tanzania na Uganda ni wanachama .

 

Miongoni mwa mambo ambayo viongozi hao wamezungumzia ni maendeleo ya uchimbaji mafuta katika Uganda na faida za mafuta hayo kwa Tanzania na kwa nchi zote wanachama wa EAC wakati ukifika mafuta hayo yakaanza kutumika.

Comments are closed.