RAIS KIKWETE AMTEUA JOEL LAURENT KUWA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA ELIMU

RAIS KIKWETE AMTEUA JOEL LAURENT KUWA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA ELIMU

Like
359
0
Monday, 26 October 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Jijini Dar es salaam inaeleza kwamba Uteuzi wa Mkurugenzi huyo ulianza tangu Oktoba 18, mwaka huu.

Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi ya TEA na ndiye aliyekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu kwa muda mrefu.

Comments are closed.