RAIS KIKWETE AMTEUA VICTORIA RICHARD MWAKASEGE KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI

RAIS KIKWETE AMTEUA VICTORIA RICHARD MWAKASEGE KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI

Like
495
0
Tuesday, 15 September 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Victoria Richard Mwakasege kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi ambaye kabla ya uteuzi wake alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi.

Aidha, Rais Kikwete amemteua Msaidizi wa Rais wa Diplomasia, Balozi Samwel Shelukindo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa Rais Kikwete amemteua Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais masuala ya Diplomasia kujaza nafasi iliyoachwa na Shelukindo.

Comments are closed.