RAIS KIKWETE ATOA CHANGAMOTO KWA BUNGE LA MAREKANI KUFUNGA MASOKO YA PEMBE ZA NDOVU NA FARU DUNIANI

RAIS KIKWETE ATOA CHANGAMOTO KWA BUNGE LA MAREKANI KUFUNGA MASOKO YA PEMBE ZA NDOVU NA FARU DUNIANI

Like
268
0
Wednesday, 30 September 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa changamoto kwa Wabunge wa Bunge la Marekani kufunga masoko ya pembe za ndovu na faru duniani, kama njia yenye uhakika ya kukomesha ujangili dhidi ya wanyamapori katika nchi za Afrika na kwa haraka zaidi.

 

Aidha, Rais Kikwete amewataka Wabunge hao kuzisaidia nchi za Afrika kifedha, ili kukomesha ujangili huo kwa sababu Wabunge hao tayari wameitangazia dunia kuwa wanazo fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya ujangili.

 

Rais Kikwete ametoa changamoto hizo wakati alipohutubia  Umoja wa Wabunge wa Bunge la Marekani ambao wanalenga kulinda na kuhifadhi wanyamapori na uhifadhi duniani, kujenga umoja wa kisiasa wa kukabiliana na ujangili na kutafuta majawabu ya changamoto zinazokabili uhifadhi unaojulikana kama ICCF.

Comments are closed.