RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA KANALI MSTAAFU AYUBU SHOMARI

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA KANALI MSTAAFU AYUBU SHOMARI

Like
287
0
Monday, 31 August 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuombeleza kifo cha mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Mafia, Mkoa wa Pwani, Kanali mstaafu Ayubu Shomari Mohamed Kimbau aliyeaga dunia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

 

Katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Engeneer Evarist Ndikilo, Rais Kikwete ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa za kifo cha Mzee Kimbau ambaye kwa miaka mingi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Mafia kupitia Chama cha Mapinduzi –CCM.

 

Comments are closed.