RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE CLARA MWATUKA

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE CLARA MWATUKA

Like
356
0
Thursday, 13 August 2015
Local News

RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mheshimiwa Clara Mwatuka aliyefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara tarehe 9 Agosti, mwaka huu.

 

Kutokana na kifo cha Mbunge huyo, Rais Kikwete ametoa pole kwa familia yake kwa kumpoteza Mzazi, kwa chama cha CUF kwa kumpoteza Mwanachama na Mbunge wake, na kwa Wananchi wa Wilaya ya Masasi kwa kumpoteza aliyekuwa Mwakilishi wao Bungeni.

 

Rais Kikwete ameiomba familia ya Marehemu kuwa na uvumilivu na utulivu kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya Mzazi na mpendwa wao.

Comments are closed.