RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MZEE PETER KISUMO

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MZEE PETER KISUMO

Like
379
0
Tuesday, 04 August 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini Mzee Peter Kisumo.

Marehemu Mzee Kisumo alishawahi kuwa kiongozi wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa Chama cha CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.

Katika salamu zake Rais Kikwete amesema kwamba taifa limeondokewa na kiongozi wa kuigwa katika utumishi uliotukuka wa umma na Chama cha Mapinduzi.

 

Comments are closed.