RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA DARESALAAM KUFUATIA VIFO VYA WATU SITA KWA AJALI YA MOTO

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA DARESALAAM KUFUATIA VIFO VYA WATU SITA KWA AJALI YA MOTO

Like
532
0
Monday, 09 February 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu sita wa familia moja waliopoteza maisha kwa moto usiku wa kuamkia Jumamosi, Januari 7, mwaka huu, katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amevielezea vifo hivyo kuwa ni vya kusikitisha na kuhuzunisha sana.

KATIKA hatua nyingine, Rais Kikwete anatarajia kuanza ziara ya siku mbili ya kikazi Mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Taarifa liyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, LEONIDAS GAMA , Rais KIKWETE atawasili Mkoani humo leo na kupumzika kabla ya kuanza kazi Feb 10 katika Manispaa ya Moshi.

Katika ziara hiyo, Rais KIKWETE atafungua jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi na baadaye kuweka jiwe la msingi la wodi ya wazazi hospitalini hapo.

IMG-20150207-WA0025 unnamed (1)IMG-20150207-WA0027

 

Comments are closed.