RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA MOROGORO KUFUATIA AJALI YA BASI NA LORI

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA MOROGORO KUFUATIA AJALI YA BASI NA LORI

Like
266
0
Wednesday, 15 April 2015
Local News

RAIS JAKAYA KIKWETE,amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dokta RAJABU RUTENGWE,kutokana na vifo vya watu 18 na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya  basi na lori,iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Msimba,barabara kuu ya Morogoro-Iringa,kilometa chache kutoka Ruaha Mbuyuni na kusababisha watu 18 kuteketea kwa moto.

Dokta KIKWETE amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 18 kutokana na ajali ya barabarani iliyosababisha miili yao kuungua vibaya

Comments are closed.