RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA WILAYA YA TEMEKE

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA WILAYA YA TEMEKE

Like
301
0
Friday, 06 February 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mheshimiwa Sophia Mjema kufuatia vifo vya wanafunzi wawili wa Darasa la Nne waliofariki dunia asubuhi ya tarehe 3Mwezi huu,  katika Shule ya Msingi Unity iliyoko Mbagala, Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea baada ya gari aina ya RAV 4 kugonga ukuta wa darasa walilokuwemo wanafunzi hao ambapo wanafunzi wengine watatu walijeruhiwa.

Rais Kikwete amewataka Wazazi wa Watoto hao wawe na moyo wa uvumilivu na subira wakati huu mgumu kwao wanapoomboleza msiba wa watoto wao.

Comments are closed.