RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI NLD

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI NLD

Like
218
0
Friday, 16 October 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amekitumia Chama cha Siasa cha National League for Democracy (NLD) salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Mheshimiwa Dkt. Emmanuel Makaidi ambaye ameaga dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Lindi .

 

Katika salamu zake hizo rais kikwete amesema  kwa hakika, NLD imepoteza mhimili wake lakini pia  Taifa limepoteza kiongozi mzuri na shupavu wa siasa katika kipindi ambacho alihitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

 

Rais Kikwete amesema  Wakati wote wa maisha yake Dokta Makaidi alionyesha uongozi wa hali ya juu na uzalendo kwa nchi yake tokea alipokuwa kiongozi hodari wa michezo hadi alipolitumia taifa  kama Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Comments are closed.