RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewaasa wabunge wa Bunge la Msumbiji kufanya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao.
Rais Kikwete ametoa ushauri huo wakati wa mazungumzo na Spika wa Bunge la Msumbiji Bibi Veronica Macamo ofisini kwake.
Rais Kikwete amewaasa wabunge wasikubali nchi yao kuingia katika vita na badala yake wakae pamoja na kuweka makubaliano ambayo yatakubalika kwa vyama vyote na hatimaye kuwaepushia wananchi wa Msumbiji kuingia kwenye vita kwa mara nyingine.