Tukio hilo la kihistoria linahitimisha mchakato wa kikao cha Bunge maalum la Katiba kilichomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuipitisha katiba tarajiwa kwa zaidi ya theluthi mbili ambapo kwa sasa inasubiri kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni hapo mwakani.
Huku katiba hiyo mpya iliyopendekezwa ikitarajiwa kuwasilishwa kwa rais baadaye hii leo, suala la kutojumuishwa moja kwa moja kwa mahakama ya kadhi katika katiba hiyo linaendelea kuwakera baadhi pamoja na serikali kuahidi kuliwasilisha bungeni kwa majadiliano zaidi hapo baadaye.