RAIS KIKWETWE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUOMBOLEZA KIFO CHA KATIBU UVCCM ARUMERU

RAIS KIKWETWE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUOMBOLEZA KIFO CHA KATIBU UVCCM ARUMERU

Like
414
0
Tuesday, 04 November 2014
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi –CCM, Taifa, Pofesa JAKAYA MRISHO KIKWETE amemtumia Salamu za Rambirambi Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM -UVCCM Taifa, SIXTUS MAPUNDA kuomboleza kifo cha Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, LUCY BONGELE kilichotokea tarehe 2 Novemba, mwaka huu kwa ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea Wilaya ya Ngorongoro baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Land Cruiser Prado Namba T380 ADP kuacha njia na kupinduka wakati Katibu huyo na Viongozi wenzake wa UVCCM walipokuwa wakienda kumsimika BRUNO KAWASANGE kuwa Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro.

Ajali hiyo iliwajeruhi Viongozi Wengine watano wa UVCCM pamoja na Dereva.

Rais KIKWETE amewaomba ndugu na jamaa wa Marehemu Lucy Bongele wawe wavumilivu na wenye subira wakati huu wanapoomboleza kifo cha mpendwa wao.

 

Comments are closed.