RAIS MAGUFUFULI KUHUDHURIA MKESHA WA KUIOMBEA AMANI TANZANIA

RAIS MAGUFUFULI KUHUDHURIA MKESHA WA KUIOMBEA AMANI TANZANIA

Like
334
0
Tuesday, 29 December 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  dokta John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha wa kuiombea amani  Tanzania  utakaofanyika Disemba 31 mwaka huu katika uwanja wa Taifa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste nchini (TFC) Godfrey Malassy Cmaandalizi yote yamekamilika ikiwemo kibali kutoka polisi.

Askofu Malassy ameongeza kuwa mkesha huo  utakuwa ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuijalia Tanzania kumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa Amani na utulivu, pamoja na Dua maalum ya kumuombea Rais.

Comments are closed.