RAIS MAGUFULI AKABIDHI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE

RAIS MAGUFULI AKABIDHI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE

Like
354
0
Friday, 18 March 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli amekabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa Hospitali ya wilaya ya Chalinze mkoani Pwani ikiwa ni utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi-CCM-kwa wananchi wa Jimbo hilo.

Akikabidhi gari hilo leo Ikulu Jijini Dar es salaam kwa mbunge wa Jimbo la Chalinze mheshimiwa Ridhiwani Kikwete kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Rais ikiwa ni kuitikia wito wa utekelezaji wa ilani ya kuboresha Afya kwa wananchi wote.

Aidha Ilomo amewataka viongozi wa wilaya na Hospitali hiyo kulitumia gari hilo kwa madhumuni maalumu ya kuwahudumia wananchi na sio vinginevyo.

Comments are closed.