RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA SUMAYE HOSPITALI

RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA SUMAYE HOSPITALI

Like
390
0
Monday, 11 January 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. John Pombe Magufuli, amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Frederick Sumaye leo, ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

 

Mheshimiwa Frederick Sumaye alilazwa katika Taasisi hiyo siku nne zilizopita kwa matibabu ya moyo na madaktari wanaomtibu wamemhakikishia Rais Magufuli kuwa anaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofikishwa katika Taasisi hiyo.

 

Katika hatua nyingine, Rais John Magufuli amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana huko Maryland Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema mwezi huu.

AM-POMBE-II

Comments are closed.