RAIS MAGUFULI APOKEA SALAMU ZA PONGEZI KUTOKA KWA MALKIA ELIZABETH II

RAIS MAGUFULI APOKEA SALAMU ZA PONGEZI KUTOKA KWA MALKIA ELIZABETH II

Like
255
0
Monday, 16 November 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Katika salamu hizo Malkia Elizabeth amemueleza Rais dokta Magufuli kuwa  anatumaini mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea kuwa mazuri wakati wa utawala wake.

 

Katika hatua nyingine Mfalme Akihito wa Japan amemueleza Mheshimiwa Magufuli nchi yake ipo tayari kuhakikisha inadumisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

Comments are closed.