RAIS MAGUFULI APONGEZWA KWA KUHAMASISHA USAFI

RAIS MAGUFULI APONGEZWA KWA KUHAMASISHA USAFI

Like
279
0
Thursday, 10 December 2015
Local News

BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaongoza  Watanzania katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika kwakufanya usafi jana, wanasiasa, wachambuzi na wananchi mbalimbali wamepongeza hatua hiyo na kuwataka watanzania kuitumia  kama mfano wa wao kuendeleza utamaduni huo wa kufanya usafi.

Wakizungumza na Efm kwa nyakati Tofauti leo, wamesema kitendo cha usafi kilichofanyika jana kimewakumbusha uongozi wa enzi za Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye aliwashirikisha wananchi wote kwa kila hatua za maendeleo.

Wamesema hatua hiyo itarejesha uzalendo miongoni mwa watanzania ambao umepotea kwa kipindi kirefu sasa.

Comments are closed.