RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

Like
309
0
Thursday, 28 April 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, Bi Juliet Kairuki.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa leo na kusainiwa na Katibu Mkuu, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, Uteuzi wa Bi Kairuki umetenguliwa kuanzia April 24 mwaka huu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa na Mheshimiwa Rais baada ya kupata taarifa kwamba Mkurugenzi huyo amekuwa hachukui mshahara wa Serikali tangu alipoajiriwa mwezi April mwaka 2013 mpaka sasa, jambo ambalo linazua maswali mengi.

Comments are closed.