Rais Magufuli ateua Kamishna mpya wa Magereza

Rais Magufuli ateua Kamishna mpya wa Magereza

Like
789
0
Friday, 13 July 2018
Local News

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais leo July 13, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza.

Uteuzi huu umeanza leo July 13, 2018.

Kabla ya uteuzi huu Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga, DSM.

Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike anachukua nafasi ya Dkt. Juma Alli Malewa ambaye amestaafu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *