RAIS MAGUFULI ATOA ZAWADI KWA WATU WALIO KATIKA MAKUNDI MAALUM

RAIS MAGUFULI ATOA ZAWADI KWA WATU WALIO KATIKA MAKUNDI MAALUM

Like
255
0
Tuesday, 22 December 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John  Magufuli,  ametoa zawadi  ya vitu mbalimbali ikiwemo vyakula vyenye thamani   ya Shilingi  milioni  8  kwa watu walio katika makundi  maalum wakiwemo watoto wanaoishi katika  mazingira hatari.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Rais, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira  Mushi  amesema zawadi hizo zinalenga kuwasaidia makundi hayo kusherehekea sikukuu kwa furaha kama watu wengine.

Amevitaja baadhi ya vituo hivyo kuwa ni  Makao ya Taifa ya watoto yatima Kurasini, mahabusu ya watoto Upanga, Makao ya Wazee na wasiojiweza  Nunge Kigamboni na Chuo  cha Ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo.

Comments are closed.