RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA INSPECTA GERALD RYOBA

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA INSPECTA GERALD RYOBA

Like
348
0
Wednesday, 06 January 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa Nchini IGP Ernest Mangu kufuatia kifo cha msaidizi wake Inspekta – Gerald Ryoba aliyepoteza maisha katika ajali ya kusombwa na mafuriko ya maji wakati akikatiza katika eneo la Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

 

Katika ajali hiyo iliyotokea Januari 3 mwaka huu, Inspekta Ryoba akiwa na Mkewe na watoto wake wawili, pamoja na watu wengine wawili walikuwa wakisafiri kutoka Geita kuja Jijini Dar es Salaam na walipofika katika eneo la Bwawani gari walilokuwa wakisafiria lilisombwa na maji na wote sita kupoteza maisha.

Comments are closed.