Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mwenyekiti wa NHC na Kuvunja Bodi ya NHC

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mwenyekiti wa NHC na Kuvunja Bodi ya NHC

Like
414
0
Wednesday, 21 March 2018
Global News

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation – NHC) Bi. Blandina Nyoni kuanzia leo tarehe 21 Machi, 2018.

Pia Mhe. Rais Magufuli ameivunja Bodi ya NHC kuanzia leo.

Uteuzi wa Mwenyekiti na bodi nyingine utafanyika baadaye.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

21 Machi, 2018

Comments are closed.