RAIS MAGUFULI AVUNJA BODI YA BANDARI NA KUTENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI

RAIS MAGUFULI AVUNJA BODI YA BANDARI NA KUTENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI

Like
364
0
Monday, 07 December 2015
Local News

KUTOKANA na utendaji mbovu wa Mamlaka ya Bandari kwa muda mrefu bila hatua zozote kuchukuliwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amevunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Joseph Msambichaka na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Awadhi Massawe.

 

Aidha Mheshimiwa Rais ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dokta Shaban Mwinjaka kuanzia leo hadi atakapopangiwa kazi nyingine.

 

Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara za kushitukiza zilizofanywa na Waziri Mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa katika Bandari ya Dar es salaam ikiwemo ile ya Novemba 27 mwaka huu na kubaini uwepo wa mwanya wa ukwepaji kodi kwa makontena 329 yaliyopitishwa bandarini kinyume na utaratibu.

Comments are closed.