RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA WANNE NA NAIBU WAZIRI MMOJA

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA WANNE NA NAIBU WAZIRI MMOJA

Like
380
0
Monday, 28 December 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wanne  na Naibu waziri mmoja aliowateua Tarehe 23 Desemba, mwaka huu.

 

Mawaziri hao wapya ni Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge,  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Yusuf Masauni.

 

Rais Magufuli pia alifanya uhamisho wa Waziri mmoja ambaye ni Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Comments are closed.