RAIS MAGUFULI AWAAPISHA RASMI WAKUU WA MIKOA 26

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA RASMI WAKUU WA MIKOA 26

Like
256
0
Tuesday, 15 March 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta John pombe Magufuli amewaapisha rasmi wakuu wa mikoa 26 wa Tanzania Bara aliowateua machi 13 mwaka huu.

Hafla ya kuwaapisha wakuu hao wa mikoa imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya wakuu wa mikoa walioapishwa leo ni pamoja na Mheshimiwa Said Meck Sadiki ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Paul Makonda mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na dokta Rehema Nchimbi mkuu wa mkoa wa Njombe.

Comments are closed.