RAIS MAGUFULI AWAAPISHA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI NA WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI NA WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI

Like
458
0
Monday, 13 June 2016
Local News

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri.

Jumamosi iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

MIC2

PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Bwana Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Mawaziri hao walikula kiapo cha uaminifu kwa rais na jamhuri ya tanzania saa tatu asubuhi katika ikulu ya rais jijini Dar es salaam.

MIC

PICHA: PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimuapisha Mh. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.