RAIS MAGUFULI KUONGOZA WATANZANIA KULIOMBEA AMANI TAIFA LEO

RAIS MAGUFULI KUONGOZA WATANZANIA KULIOMBEA AMANI TAIFA LEO

Like
273
0
Thursday, 31 December 2015
Local News

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JOHN POMBE MAGUFULI leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha wa kuiombea amani Tanzania utakaofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste nchini -TFC GODFREY MALASSY amesema kuwa mkesha huo utakuwa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuijalia Tanzania kumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi oktoba mwaka huu kwa Amani na utulivu, pamoja na Dua maalum ya kumuombea Rais.

Aidha ameeleza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na uuzwaji wa kitabu cha ijue siri ya amani ya Taifa ambapo pesa zitakazopatikana kutokana na kitabu hicho zitapelekwa kwenye makundi ya watu wenye mahitaji maalumu.

Comments are closed.