RAIS MAGUFULI NA MITANDAO YA KIJAMII

RAIS MAGUFULI NA MITANDAO YA KIJAMII

Like
399
0
Wednesday, 13 July 2016
Local News

Rais John Magufuli ametumia dakika 40 kuelezea jinsi alivyokuwa akilala usiku wa manane kuchambua majina 185 ya wakurugenzi wa wilaya, amesema matokeo yake hakuna “vilaza” waliopenya, akijibu habari zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika hotuba yake Rais alisema katika kazi hiyo iliyomchukua takribani miezi minne, alipitia jina la kila mkurugenzi aliyemteua na hakuna aliyepenyeza jina lake kutaka kuteuliwa likapita. “Aliyejaribu, jina lake liliondolewa. Sikujua hata sura zenu ila kwa jinsi ninavyoziona nyuso zenu hapa, hakika ninyi ni watu sahihi,” amesema Rais Magufuli wakati wa hafla ya kiapo kwa wakurugenzi hao iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mitandao ya kijamii ilikuwa kwenye mjadala wa elimu ya wateule hao iliyotawaliwa na makada walioshindwa katika hatua za ndani ya CCM kwenye kinyang’anyiro cha ubunge mwaka jana, vikisema baadhi walikuwa na vyeti vya kughushi na wengine elimu chini ya shahada ya kwanza. “Lazima niseme kwa dhati kwamba process za kuwapata nyinyi zimechukua zaidi ya miezi minne,” alisema Rais. “Kwa hiyo tulianza uchambuzi wa kina kwelikweli, mmepitia katika milolongo mingi kwelikweli. Vyombo mbalimbali vimehusika kwelikweli. “Lengo lilikuwa ni moja tu; ninataka kujenga Tanzania ya aina gani? Na je, nichague watu wa aina gani watakaoifikisha hiyo Tanzania ninayoitaka na ndio maana process ilikuwa ndefu.” Rais Magufuli pia alidokeza kuhusu habari hizo za kwenye mitandao. “Na ndio maana saa nyingine, ninapojaribu kuingia kwenye mitaandao, ninaona comment (maoni) nyingine, nacheka wee,” alisema na kuibua kicheko kutoka kwa wateule na wageni wengine waliofika Ikulu. “Mara mwingine anazungumza jina la fulani, yeye anafanya hotelini. Majina kufanana si kosa. Anasema ana certificate (cheti) ya hoteli. Mimi najua niliyemteua kwa jina hilo, ana masters ya MBA (shahada ya uzamili ya uongozi wa biashara).

Comments are closed.