RAIS MPYA WA AFGHANSTAN ASAINI MKATABA NA NATO

RAIS MPYA WA AFGHANSTAN ASAINI MKATABA NA NATO

Like
654
0
Tuesday, 30 September 2014
Global News
afughan2

Ashraf Ghani rais mpya wa Afghanstan

Siku moja baada ya kuapishwa kuwa rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani, serikali yake imetia saini mkataba mpya wa usalama na shirika la kujihami la NATO.

Mkataba huo utaidhinisha zaidi ya wanajeshi elfu kumi na mbili, wengi wakiwa wamarekani, kusalia nchini Afghanistan hata baada ya kumalizika kwa kandarasi yao mwaka huu.

Mkataba huo ulitiwa sahihi katika hafula iliyotangazwa moja kwa moja katika televisheni na mshauri wa maswala ya usalama wa kitaifa wa Afghanistan Hanif Atmar na balozi wa Marekani nchini humo Jim Cunningham, huku Rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani akishuhudia.

 

afughan

Rais aliyeondoka Hamid Karzai alikataa kwa muda mrefu kusaini mkataba wa kuwaongezea wanajeshi wa Marekani muda wa kukaa huko, na hivyo kusababisha mvutano kati yake na Marekani.

Bwana Karzai alikuwa anasisitiza kuwa la muhimu zaidi ni kuanzisha mpango wa amani na kusitisha mapigano na wanamgambo wa Taleban.

Vikosi vya NATO vimekuwa vikipunguzwa nchini Afghanistan na taratibu kurudisha udhibiti wa usalama wa nchi hiyo kwa vikosi vya Afghanistan.

 

Comments are closed.