Rais Trump kumualika Putin Washington

Rais Trump kumualika Putin Washington

Like
377
0
Friday, 20 July 2018
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump anakusudia kumwalika
Washington, Rais wa Urusi Vladmir Putin baadaye mwaka huu, licha
ya kuendelea kuwepo ukosoaji juu ya mkutano wao uliofanyika
Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Finland Helsinki.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sara Sanders amesema majadiliano
kuhusiana na ziara hiyo tayari yameanza.
Hata hivyo, Kiongozi wa maseneta kupitia chama cha Democrat
nchini humo Chuck Schumer ameupinga mualiko huo mara moja
kwa kusema kuwa Rais Trump hapaswi tena kukutana ana kwa ana
na Rais Putin mpaka pale Wamarekani watakapojua nini kilitokea
katika mkutano wa Helsinki.
Awali katika mkutano wake na kituo cha televisheni cha CNBC Rais
Trump alitetea tena msimamo wake wa kuimarisha mahusiano na
Urusi, lakini amesema kama jambo hilo halitafanikiwa, atakuwa adui
na Rais huyo wa Urusi kushinda ilivyokuwa awali.
Wakati huohuo taarifa hizo za mualiko wa Rais Putin, zimeonekana
kumshangaza Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Marekani Dan
Coats, ambaye aliambiwa jambo hilo katika mahojiano ya moja kwa
moja wakati wa mkutano wa usalama uliofanika katika jimbo la
Colorado.
Alijibu kwa kucheka na kusema kuwa ''..hilo litakuwa la namana ya
pekee''
Ameongeza kusema kuwa bado hajafahamu nini walichojadili Rais
Putin na Trump katika mkutano wao, ambao ulihudhuriwa tu na

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *