RAIS WA GABON AAHIDI KUTOA URITHI WAKE WOTE KWA VIJANA

RAIS WA GABON AAHIDI KUTOA URITHI WAKE WOTE KWA VIJANA

Like
228
0
Tuesday, 18 August 2015
Global News

RAIS wa Gabon Ali Bongo Ondimba ameahidi kutoa urithi wake wote kwa vijana nchini humo.

Rais Bongo amesema kuwa mali yote aliyopokea kama urithi kutoka kwa babaake mzazi aliyekuwa rais wa Gabon kwa kipindi kirefu,Omar Bongo itakwenda kwa vijana wa Gabon.

Shirika la habari la AFP limesema kuwa rais Bongo ameahidi kuuza majengo mawili yaliyopo Ufaransa aliyopewa na mzazi kwa thamani ya Franka moja kama ishara ya kujitolea kuimarisha hali ya kiuchumi ya vijana wa taifa hilo.

Comments are closed.