RAIS WA GABON AITUHUMU UFARANSA

RAIS WA GABON AITUHUMU UFARANSA

Like
166
0
Tuesday, 15 September 2015
Global News

RAIS wa Gabon Ali Bongo amesema kuwa kukamatwa kwa mkuu wa majeshi wa Taifa hilo mjini Paris mnamo mwezi Agosti mwaka huu ni jaribio la kuifedhehesha Gabon.

Rais Bongo alikuwa akizungumza katika makao rasmi ya rais Francois Hollande baada ya kukutana naye mjini Paris.

Mkuu huyo wa majeshi aliyekamatwa Maixent Accrombessi alizuiliwa kwa muda katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle kwa tuhuma za ufisadi baada ya kandarasi ya sare za kijeshi nchini Gabon kupewa kampuni moja ya Ufaransa kulingana na chombo cha habari cha AFP.

Comments are closed.