RAIS WA IRAN AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UINGREZA

RAIS WA IRAN AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UINGREZA

Like
219
0
Tuesday, 25 August 2015
Local News

WAZIRI wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond amekutana na rais wa Iran Hassan Rouhani mjini Tehran kwaajili ya mazungumzo ya kiserikali baina ya nchi hizo mbili.

Waziri Hammond amesema Iran ina ushawishi mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati na inaweza kuwa mshirika mojawapo muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Amesema mataifa hayo mawili yana msimamo wa pamoja licha ya historia ya kutoaminiana na yamekubaliana juu ya hoja ya kulishinda kundi la Dola la Kiislamu na kuzuia mihadarati kutoka Afghanistan isifike Ulaya.

 

Comments are closed.