RAIS WA IRELAND ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA MAGUFULI

RAIS WA IRELAND ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA MAGUFULI

Like
283
0
Friday, 20 November 2015
Local News

RAIS wa Ireland, Michael Higgins amemtumia Salamu za Pongezi  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya Tano.

Katika Salamu zake hizo, Rais Higgins amesema Ireland na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri na wa kirafiki kwa miaka mingi, hivyo ana matarajio kwamba katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli, uhusiano huo utaimarishwa zaidi.

Katika hatua nyingine Rais wa  Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Robert Mugabe amemtumia Salamu za Pongezi Mheshimiwa Dokta Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 2015.

Comments are closed.