RAIS WA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI AONYA KUHUSU UCHAGUZI

RAIS WA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI AONYA KUHUSU UCHAGUZI

Like
199
0
Friday, 30 October 2015
Global News

Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, ameonya kuwa maadui wa Amani wanaojaribu kuzuia uchaguzi mkuu nchini humo usifanyike mwezi Disemba.

 

Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Septemba lakini ukaahirishwa baada ya kuzuka tena kwa makabiliano kati ya Wakristo na Waislamu na kusababisha watu 40 kuawa.

 

Hata hivyo Rais Samba amesema suluhu pekee ya kumaliza matatizo hayo ni kuwa na serikali halali iliyochaguliwa na raia.

Comments are closed.