RAIS WA MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 26 YA TANZANIA BARA

RAIS WA MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 26 YA TANZANIA BARA

Like
341
0
Monday, 25 April 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, leo amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania bara.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, wawili wamebadilishiwa vituo na 13 wamebakishwa katika vituo vyao vya sasa.

Makatibu tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano April 27, Ikulu saa tatu asubuhi.

Comments are closed.