RAIS WA MSUMBIJI AAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA NCHI HIZI MBILI

RAIS WA MSUMBIJI AAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA NCHI HIZI MBILI

Like
165
0
Tuesday, 19 May 2015
Local News

RAIS wa Msumbiji mheshimiwa FILIPE NYUSSI ameahidi kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ili kuleta manufaa ya kutosha kwa wananchi wan chi hizo mbili.

Rais NYUSSI ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akiwahutubia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni hatua ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu aliyoifanya nchini tangu mei 17 mwaka huu.

Mbali na hayo mheshimiwa NYUSSI amewaasa watanzania kuilinda na kuiendeleza amani iliyopo kwa kuwa ni hazina muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote duniani.

Comments are closed.