RAIS WA MYNAMAR AAMURU WAFUNGWA 101 KUACHIWA HURU

RAIS WA MYNAMAR AAMURU WAFUNGWA 101 KUACHIWA HURU

Like
228
0
Friday, 22 January 2016
Global News

RAIS wa Myanmar anayemaliza muda wake, Thein Sein, ameamuru kuachiwa huru kwa wafungwa 101 wakiwemo takribani 25 waliohukumiwa kwa makosa ya kisiasa.

 

Maafisa nchini humo wamesema msamaha huo unawahusu pia wafungwa 77 waliokuwa wamehukumiwa kifo na adhabu yao kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha.

 

Kwa mujibu wa chama cha wafungwa wa kisiasa  nchini humo, miongoni mwa wafungwa 25 wa kisiasa, yumo raia wa New Zealand, Philip Blackwood, ambaye alihukumiwa mwezi Machi kwa kosa la kwenda kinyume na misingi ya kidini.

Comments are closed.