RAIS WA UFARANSA ADAI URUSI INAPASWA KUONDOLEWA VIKWAZO

RAIS WA UFARANSA ADAI URUSI INAPASWA KUONDOLEWA VIKWAZO

Like
292
0
Monday, 05 January 2015
Global News

RAIS WA UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE amesema kuwa vikwazo vya nchi za Magharibi vinavyoendelea kuiathiri Urusi vinapaswa kuondolewa kama hatua zitapigwa katika ufumbuzi wa mgogoro wa Ukraine.

HOLLANDE amekiambia kituo kimoja cha Radio nchini Ufaransa kuwa anatarajia kupatikana mafanikio katika mazungumzo ya Kimataifa yanayopangwa nchini Kazakhstan mnamo Januari 15 katika juhudi mpya za kushinikiza mpango wa amani, ambapo kiongozi wa Ukraine anayeungwa mkono na nchi za Magharibi Rais PETRO POROSHENKO anatarajiwa kukutana na Rais VLADMIR PUTIN wa Urusi.

Comments are closed.