RAIS wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi amemfukuza kazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Khaled Bahah kutokana na kile alichoeleza utendaji mbovu ndani ya serikali.
Mabadiliko haya yanakuja ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa hatua ya kusimamishwa mapigano kati ya pande mbili zinazohasimiana katika mgogoro nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la serikali nchini humo, Rais Hadi amemteua Ahmed Obaid bin Daghr kuwa waziri mkuu huku akimteua Meja Jenerali Ali Mohsen Al -Ahmar kuwa makamu wa Rais.